Tuesday, June 19, 2012

Baraza la wawakilishi lafunguka: Tusilazimishane katika muungano huu. Watanganyika wanatuhadaa Written by Ashakh (Kiongozi) // 18/06/2012 // Habari // 11 Comments wanabodi. Amini Usiamini UAMSHO sio UAMSHO tena. yaani Licha ya Vyombo vya habari kuripoti na kupotosha kuhusu UAMSHO. Ndani ya baraza la wawakilishi ni kinyume kabisa, hakuna mwakilishi anaejaribu kulizungumzia, na hata akijaribu kuligusa ni wazi unaweza ukahisi kama analiunga MKono japo sio moja kwa moja. Katika hali isiyotarajiwa na wengi. Leo hii Wazanibar wametoa madai mazito kuhusu muungano unavyoendeshwa huku Lawama za wazi wazi zikilekezwa kwa Watanganyika kwamba wanawahadaa wazanzibar Hoja zenyewe: 1) Mh Raza: Ilikuwa ni vigelegele, makofi na hata vicheko vilitanda kila kona barazani huku Spika na Mawaziri wa SMZ wakionekana wazi kupigwa na Butwaa. Nini Alisema Mh Raza: No1: “Mh Spika, nina nyaraka za makubaliano kati ya Serekali ya Awamu ya 3 ya Dk Salmini na Mh Mkapa kuhusu Zanzibar kujiunga OIC. Haya sio maneno ya Mitaani, ninazo nyaraka za makubaliano, na kama serekali ya sasa wanahizaji nitawapa ambazo wenzetu walisema Tanzania itajiunga OIC kwa manufaa ya Zanzibar. Lkn wenzetu wametuhada na wanaendelea kutuhadaa. huku wao wakiwa na UBALOZI wa vertican kwa manufaa yao. Hi ni hadaa kubwa tunayoendelewa kufanyiwa Zanzibar, Hatukubali tena tunasema hatukubali, kwa muungano wa aina hii ” makofi ukumbi mzima. eti tunaambiwa kupata uanachama wa OIC ni kazi kubwa, naimba serekali hii kazi inepe mimi, ndani ya miezi 3 Tanzania itajiunga na OIC ili tutengezewe madaraja, barabara na vyuo vikuu kama baadhi ya nchi. Zanzibar tunanjaa wao kama Watanzania bara wameshiba waache washibe No2: “Mh Spika, niliwahi kusema huko Nyuma, itafika siku vyeti vya ndoa tutakiwa tuvifate Dodoma, nikapuuzwa. sasa unaona, waziri wa nishati wa Tanzania bara leo ndio anawakilisha Wazanzibar ktk jumuia ya Afrika Mashariki huku Waziri huyo akiwa mwisho wake ni CHUMBE tu. hii ni hadaa kubwa tunayohadaiwa wazanzibar huku viongozi wetu wakiwa sio wakweli , sijui nini wanachoogopahili tunasema Tunashachoka, hatulitaki litendeke ” No3: Mh spika, miaka 48 ya Muungano hadi kuna watu ndani ya tanganyika wanatuona Zanzibar hatuna maana, leo mawaziri wanakubaliana kutatua tatizo la Muunagno, kuna watu wenye nia mbaya na Zanzibar wanazuia. Muungano kama huu haufai, huu si Muungano, huu ni ulaghai” Makofi. Mwakilishi wa Kitope “Mimi naona sasa hakuhitajiki viongozi wasomi kutatua matatizo ya Muungano, tuachaguliwe sisi wasio na Elimu wenye kutoa kauli. maana ndugu zetu hawataki kutusikia. KWA UFUPI KILA MWAKILISHI INAOENAKANA ANAKWERA NA MUUNGANO HUU UNAVYOENDESHWA licha ya waziri Aboud kudai watu wasubiri katiba mpya. sio CCM SIO CUFSerikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Makamo wa Pili wa Rais pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mohamed Aboud Mohamed ilipiga marufuku harakati za Uamsho na jumuiya nyengine za kuendesha Mihaadhara ya kujadili hatma na masuala ya Muungano wakati tume ya Kukusanya na kuratibu maoni tayari imeshazinduliwa na Rais. Tume hii ndiyo iliyopewa madaraka ya kusimamia utaratibu wote wa kukusanya maoni pamoja na kuandaa au kuyapa Baraka makongamano, mikusanyiko na harakati za kukusanya maoni haya. Amri hii imepelekwa kwenye vyombo vya Sheria kwa utekelezaji na na tayari tumesikia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba alivyopiga marufuku mikusanyiko na huku Uamsho kutoa tamko rasmi kupingana na amri hii kwamba imekwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar inayowapa haki ya uhuru wa kuabudu na kueneza dini. Pia baada ya machafuko mwezi Mei na kutokea na uvunjifu wa amani Serikali kupitia vyombo vya ulinzi umeonekana kulifanyia kazi suala hili kisawa sawa kwa kuzuia Mihadhara na mikusanyiko ya kikundi cha uamsho. Kipengele kinachotumika kuipa nguvu tume ni ibara 18(6) kinachoitaka tume hiyo kutoruhusu asasi, taasisi au makundi ya watu kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa wanachama wake kutoa maoni na 21(1)-(4) kinachotamka makosa mbalimbali na adhabu zake Kinachokatazwa hapa au kinachojadiliwa kwa kadri nilivyofuatilia mwendelezo wa Mihaadhara ya Uamsho mimi sikioni au sijakitambua. Labda Wanasheria mnielimishe. Tume imepewa hadidu rejea maalum (terms of reference) na mojawapo katika hadidu rejea hizo ni kwamba suala la Muungano lisijadiliwe wala kufikiriwa kuuvunja bali kurekebishwa na kujengwa uwe imara zaidi. Uamsho wanachokizungumza katika Mihaadhara bila ya kumun’gunya maneno wala kutumia lugha ya istiara ni kwamba Muungano uvunjwe hawautaki kwa kutokuwa na maslahi kwa watu wa Zanzibar. Wanachokikusanyia maoni tume ni kitu chengine ambacho kinaelekea katika kupata Katiba mpya ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania 2014 na wanachokihubiri Uamsho ni kitu chengine kabisa. Hivyo wamevunja sheria gani? Wanakatazwa kuendeleza Mihaadhara yao kwa kipengele kipi? Uamsho wanawaelimisha waumini kwamba Muungano hauna maslahi kwayo hivyo utafutiwe njia ya kuuvunja iwe ya moja kwa moja au kwa kupitia kura ya maoni ambayo wataulizwa wananchi kama wanautaka Muungano huu au hawautaki. Sasa tukiwataka wakaombe kibali cha kuzungumza haya kutoka kwa tume ya Kukusanya maoni kwa msingi gani kwani hili halimo katika hadidu rejea za Tume. Kwa viongozi kutoa kauli za vitisho dhidi ya wasioutaka Muungano ni kuibeza Demokrasia kwa kisingizio cha kulinda amani na utulivu wa nchi na pia kutaweza kuhatarisha mchakato mzima wa ukusanywaji wa maoni kuonekana haukuwa huru na haki kama Rais Kikwete alivyoagiza na Tume ilivyojizatiti kwamba itakuwa huru kupokea maoni yoyote. Kama khofu ni kwamba harakati hizi zinaweza kuathiri saikolojia ya watakaotoa maoni kwa kuvutika na hoja za Uamsho hii ni khofu isiyokuwa na mashiko ya kukamatia. Uamsho hawafanyi kampeni wala kwa fikra zangu hawakuwa na haja ya kutoa tamko lolote kwani vipengele vya kisheria vinavyozungumzwa na tume haviwagusi wanauamsho kwa njia yoyote. Walipaswa kuwakabili waliokataza na kutaka ufafanuzi kwa vigezo gani na vipi shughuli zao zinakwazwa na vipengle vya tume ya Kuratibu maoni ya Katiba. Waachieni Uamsho waendelee na shughuli zao

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Makamo wa Pili wa Rais pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mohamed Aboud Mohamed ilipiga marufuku harakati za Uamsho na jumuiya nyengine za kuendesha Mihaadhara ya kujadili hatma na masuala ya Muungano wakati tume ya Kukusanya na kuratibu maoni tayari imeshazinduliwa na Rais.
Tume hii ndiyo iliyopewa madaraka ya kusimamia utaratibu wote wa kukusanya maoni pamoja na kuandaa au kuyapa Baraka makongamano, mikusanyiko na harakati za kukusanya maoni haya.
Amri hii imepelekwa kwenye vyombo vya Sheria kwa utekelezaji na na tayari tumesikia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba alivyopiga marufuku mikusanyiko na huku Uamsho kutoa tamko rasmi kupingana na amri hii kwamba imekwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar inayowapa haki ya uhuru wa kuabudu na kueneza dini.
Pia baada ya machafuko mwezi Mei na kutokea na uvunjifu wa amani Serikali kupitia vyombo vya ulinzi umeonekana kulifanyia kazi suala hili kisawa sawa kwa kuzuia Mihadhara na mikusanyiko ya kikundi cha uamsho.
Kipengele kinachotumika kuipa nguvu tume ni ibara 18(6) kinachoitaka tume hiyo kutoruhusu asasi, taasisi au makundi ya watu kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa wanachama wake kutoa maoni na 21(1)-(4) kinachotamka makosa mbalimbali na adhabu zake
Kinachokatazwa hapa au kinachojadiliwa kwa kadri nilivyofuatilia mwendelezo wa Mihaadhara ya Uamsho mimi sikioni au sijakitambua. Labda Wanasheria mnielimishe.
Tume imepewa hadidu rejea maalum (terms of reference) na mojawapo katika hadidu rejea hizo ni kwamba suala la Muungano lisijadiliwe wala kufikiriwa kuuvunja bali kurekebishwa na kujengwa uwe imara zaidi.
Uamsho wanachokizungumza katika Mihaadhara bila ya kumun’gunya maneno wala kutumia lugha ya istiara ni kwamba Muungano uvunjwe hawautaki kwa kutokuwa na maslahi kwa watu wa Zanzibar.
Wanachokikusanyia maoni tume ni kitu chengine ambacho kinaelekea katika kupata Katiba mpya ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania 2014 na wanachokihubiri Uamsho ni kitu chengine kabisa. Hivyo wamevunja sheria gani? Wanakatazwa kuendeleza Mihaadhara yao kwa kipengele kipi?
Uamsho wanawaelimisha waumini kwamba Muungano hauna maslahi kwayo hivyo utafutiwe njia ya kuuvunja iwe ya moja kwa moja au kwa kupitia kura ya maoni ambayo wataulizwa wananchi kama wanautaka Muungano huu au hawautaki. Sasa tukiwataka wakaombe kibali cha kuzungumza haya kutoka kwa tume ya Kukusanya maoni kwa msingi gani kwani hili halimo katika hadidu rejea za Tume.
Kwa viongozi kutoa kauli za vitisho dhidi ya wasioutaka Muungano ni kuibeza Demokrasia kwa kisingizio cha kulinda amani na utulivu wa nchi na pia kutaweza kuhatarisha mchakato mzima wa ukusanywaji wa maoni kuonekana haukuwa huru na haki kama Rais Kikwete alivyoagiza na Tume ilivyojizatiti kwamba itakuwa huru kupokea maoni yoyote.
Kama khofu ni kwamba harakati hizi zinaweza kuathiri saikolojia ya watakaotoa maoni kwa kuvutika na hoja za Uamsho hii ni khofu isiyokuwa na mashiko ya kukamatia. Uamsho hawafanyi kampeni wala kwa fikra zangu hawakuwa na haja ya kutoa tamko lolote kwani vipengele vya kisheria vinavyozungumzwa na tume haviwagusi wanauamsho kwa njia yoyote. Walipaswa kuwakabili waliokataza na kutaka ufafanuzi kwa vigezo gani na vipi shughuli zao zinakwazwa na vipengle vya tume ya Kuratibu maoni ya Katiba.
Waachieni Uamsho waendelee na shughuli zao

No comments: