Thursday, December 22, 2011

MAFURIKO DAR





NJUMBA ZILIVYO ATHIRIKA NA MVUA ILIYONYESHA DAR.




Waathirika wakipata mbili tatu baada ya harakati nzito za uokoaji wa mali zao









Hivi ndivyo baadhi ya Raia walivyo nusurika na mafiriko





Hii ni bahari kasoro mawimbi, hadi jana watu 20 wameshapoteza

Tuesday, December 20, 2011

EPIQ NATION HATARI TUPU ZANZIBAR

Wananchi mbali mbali katika Jumba la Michenzani wakiangalia promo ya Epiq Nation iliyofanyika katika uwanja wa kisonge  bila kujali usalama wa maisha yao. hata hivyo hakuna mtu yoyote alipata na tatizo hadi kumalizika kwa tamasha hilo. Jumba hilo lina kuna ukubwa wa horofa zisizo pungua tano.

KIJANA KATIKA MAUZO






KIJANA AKIWA AMEPOZI KATIKA JUMBA LA AJABU FORODHANI











HAPA KIJANA AKIANGALIA MAJI YA BAHARI YA HINDI FORODHANI ZANZIBAR
























KIJANA ANAENDELEA KUPUNGUZA MAWAZO KATIKA SEHEMU MBALI MBALI ZA KUPENDEZA









Monday, December 19, 2011


SHIDA YA USAFIRI


Baadhi ya abiria wanavyo sumbuka katika harakati za kutafuta maisha inayochangiwa na shida ya usafiri sehemu tofauti duniani

UMUHIMU WA KAZI

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Bangladesh wakihakisha kureshesha umeme ulio katika kwa muda wa dakika 5.

BAADA YA KUMALIZA KAZI

Wafanyakazi wa kampuni ya ujengaji wa daraja wakiwa wamepumzika baada ya kumaliza majukumu yao ya siku

UMRI WA COCACOLA

Hivi ndivyo chupa za Cocacola zilivyopitia katika umri wake.

Sunday, December 18, 2011

ZANZIBAR YETU

ZANZIBAR NDIO HII
Ingawa watu wengi hawafahamu vivutio viliyopo katika visiwa wa Zanzibar, ila visiwa hivi vina vitulivu vingi vya moyo, wengi wanafikiria kuwa Zanzibar ina uzuri wa fukwe za bahari tu, kumbe sio kweli majengo jenye taswira nzuri na ya kistoria. basi tudumisheni maslimali zetu sote kwa umoja



huu ni msitu wa jozani ambao upo baina ya kijiji cha Pete na Jozani, watu wengi hasa ya watalii ndani na pia wa nje hutumia katika mapumziko yao ya kila siku.

kwa kweli msitu huu una vivutio vingi ambavyo hutoweza kuvipata katika sehemu nyengine yoyote duniani. Mnyama Paa ni moja wapo wa vivutio vilivyomo katika msitu huu, paa hao ni wadogo wadogo ambao hutatikana katika sehemu hii peke yake, pia kuna kima (kima punju) ambao ni furahisho na pambo kubwa katika visiwa hivi. kwani hata tafiti

zinaonesha kwamba kima hawa ni kima wa aina yake ambao wanaowezo wa kuishi sehemu moja tu duniani ambapo ni katika visiwa vya Zanzibar.
 Huyu ni aina wa ndege ambao wanapamba mandhari hii ya msitu wa Jozani, kwa kweli kwa macho tu basi   hufurahisha na kuvutia. ukiwa katika sehemu hii utapenda usiondoke ili uweze kuangalia vivutio vingi ambavyo kwa muda mfupi utashandwa kuvimaliza.

 hii ni aina moja wapo wa kima ambao hupatikana katika usitu huu. kwa jina hawa wanaitwa kima wekundu au kima Punju. kima Punju ni jina la asili la kima hawa ambapo watu wa karibu wa vijiji vya Jozani hupenda kulitumia. pia kuna kima weusi ambao pia hupatikana katika sehemu hii, hao ni kima wa kawaida ambapo kuwa hata raia ana haki ya kuwaminiliki kima hao lengo la kuwafuga. watu wengi huwafuga katika manyumba yao kama kivutio cha manyumba hayo.
 haya ndio maisha ya kima hawa, wanapendana na pia wanapenda watu waokwenda kuwatizama,  mara nyingi hufurahi na kucheza wakiwa na watu kama vile watalii katika eneo lao, furaha yao ina maanisha kuwa ni faraja ya moyoni kuwatembelea, tabia hii ni ya kima pekee ambao ukiwaita wanakuja na kuwachezea na kucheza pamoja. ila huwa hawapendi kupigwa. kima wekundu hipekea zawadi wanazoletewa na wageni wanaokwenda kuwatizama. kwa kweli hii ni furahisho la moyo basi tembelea ukajionee wenyewe na uone wengi jaliopo katika msitu huu,
kwa kweli vivutio vilivyopo katika msitu huu ni vingi sana kushoto kwako kuna miamba, hii ni maumbile ya pango moja ambalo lipo katika kijiji cha Pete kilicho karibu sana na msitu wa Jozani, pango hilo 

 lina storia kubwa na ina mvuto wa pekee,  pango hilo lina chemchem ya maji baridi ambayo ladha yake ni
 matamu  mno, maji hayo hutiririka kutokea katika njia zake na watu wanao kwenda kutembelea hapo


 huyatumia kama kiburudisha koo. hii ndio Zanzibar yetu, njoo ufurahie maajabu mengi yaliyopo katika visiwa hivi. uongozi wa Jozani imeweka kiwango cha chini cha kuingilia katika msitu huu kwani kimezingatia haki ya mnyonge. mnyonge nawe pia unatamani kwenda katika msitu wa Jozani ili kuweza kujionea mwenyewe. basi nenda usiridhike kwa kusoma au kuhadithiwa.  kwani Jozani kuna vivutio vingi vya wanyama kama vile nyoka wakubwa  na kadhalika 








 

Friday, December 16, 2011

MAHAFALI YA CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA CHWAKA

Elewa kuwa kusoma ni haki ya binaadamu kwenye akili timamu au pungufu (taahira). katika miaka ya karibuni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi katika uanzishwaji wa chuo vikuu na vya kati ili kwenda sambamba wa utowaji wa haki kwa wanyonge, na haya sasa ndio matunda yake. hawa ni baadhi ya vijana walihitimu mafunzo katika ngazi mbali mbali katika chuo cha ZIFA kiliopo Wilaya ya kusini.








VIJANA WANAOTARAJIWA KUWA VIONGOZI WA ZANZIBAR WAKITEMBELEA JENGO JIPYA LA ZRB