Ingawa watu wengi hawafahamu vivutio viliyopo katika visiwa wa Zanzibar, ila visiwa hivi vina vitulivu vingi vya moyo, wengi wanafikiria kuwa Zanzibar ina uzuri wa fukwe za bahari tu, kumbe sio kweli majengo jenye taswira nzuri na ya kistoria. basi tudumisheni maslimali zetu sote kwa umoja
huu ni msitu wa jozani ambao upo baina ya kijiji cha Pete na Jozani, watu wengi hasa ya watalii ndani na pia wa nje hutumia katika mapumziko yao ya kila siku.
kwa kweli msitu huu una vivutio vingi ambavyo hutoweza kuvipata katika sehemu nyengine yoyote duniani. Mnyama Paa ni moja wapo wa vivutio vilivyomo katika msitu huu, paa hao ni wadogo wadogo ambao hutatikana katika sehemu hii peke yake, pia kuna kima (kima punju) ambao ni furahisho na pambo kubwa katika visiwa hivi. kwani hata tafiti
zinaonesha kwamba kima hawa ni kima wa aina yake ambao wanaowezo wa kuishi sehemu moja tu duniani ambapo ni katika visiwa vya Zanzibar.
Huyu ni aina wa ndege ambao wanapamba mandhari hii ya msitu wa Jozani, kwa kweli kwa macho tu basi hufurahisha na kuvutia. ukiwa katika sehemu hii utapenda usiondoke ili uweze kuangalia vivutio vingi ambavyo kwa muda mfupi utashandwa kuvimaliza.
hii ni aina moja wapo wa kima ambao hupatikana katika usitu huu. kwa jina hawa wanaitwa kima wekundu au kima Punju. kima Punju ni jina la asili la kima hawa ambapo watu wa karibu wa vijiji vya Jozani hupenda kulitumia. pia kuna kima weusi ambao pia hupatikana katika sehemu hii, hao ni kima wa kawaida ambapo kuwa hata raia ana haki ya kuwaminiliki kima hao lengo la kuwafuga. watu wengi huwafuga katika manyumba yao kama kivutio cha manyumba hayo.
haya ndio maisha ya kima hawa, wanapendana na pia wanapenda watu waokwenda kuwatizama, mara nyingi hufurahi na kucheza wakiwa na watu kama vile watalii katika eneo lao, furaha yao ina maanisha kuwa ni faraja ya moyoni kuwatembelea, tabia hii ni ya kima pekee ambao ukiwaita wanakuja na kuwachezea na kucheza pamoja. ila huwa hawapendi kupigwa. kima wekundu hipekea zawadi wanazoletewa na wageni wanaokwenda kuwatizama. kwa kweli hii ni furahisho la moyo basi tembelea ukajionee wenyewe na uone wengi jaliopo katika msitu huu,

lina storia kubwa na ina mvuto wa pekee, pango hilo lina chemchem ya maji baridi ambayo ladha yake ni
matamu mno, maji hayo hutiririka kutokea katika njia zake na watu wanao kwenda kutembelea hapo

huyatumia kama kiburudisha koo. hii ndio Zanzibar yetu, njoo ufurahie maajabu mengi yaliyopo katika visiwa hivi. uongozi wa Jozani imeweka kiwango cha chini cha kuingilia katika msitu huu kwani kimezingatia haki ya mnyonge. mnyonge nawe pia unatamani kwenda katika msitu wa Jozani ili kuweza kujionea mwenyewe. basi nenda usiridhike kwa kusoma au kuhadithiwa. kwani Jozani kuna vivutio vingi vya wanyama kama vile nyoka wakubwa na kadhalika
No comments:
Post a Comment